Watoto wa Hosni Mubarak waachiliwa huru

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wana wa Hosni MUbarak waachiliwa huru

Wana wawili wa aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak wameachiliwa kutoka jela, miaka minne baada ya kukamatwa na kuzuiliwa kwa pamoja na baba yao.

Wakuu wa gereza wanasema kuwa Gamal na Alaa Mubarak wote wanabiashara maarufu waliachiliwa mapema leo Jumatatu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hosni Mubarak

Juma lililopita mahakama iliamuru kuachiliwa kwao huku kesi dhidi yao kuhusu ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma, ikiendelea.

Mubarak anaendelea kuzuiliwa katika Hospitali moja ya kijeshi, ambapo anatumikia hukumu ya matumizi mabaya ya pesa za umma.