Idara ya Usalama kuvunjwa,Argentina

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Argentina Fernandez de Kirchner

Rais wa Argentine Fernandez de Kirchner ametangaza mpango wake wa kuifunga idara ya usalama nchini humo kwa madai kuwa inahusishwa na mauaji ya mwendesha mashtaka maalum Alberto Nisman jumapili wiki iliyopita.

Bi. Fernandez amesema serikali yake inatayarisha muswada utakaoiwezesha serikali hiyo kuunda idara mpya ya usalama wa taifa.

Anasema idara hiyo ilisababisha kuuawa kwa mwendesha mashitaka maalumu Alberto Nisman ambaye alikutwa ameuawa katika makazi yake muda mfupi kabla ya kuwasilisha ushahidi katika kesi inayowakibili maofisa wakuu wa serikali.

Kahsfa hiyo ni kufuatia kutuhumiwa kwa raia wa Iran aliyehusishwa na mashambulizi ya bomu huko Buenos Aires dhidi ya kituo cha Kiyahudi 1994 ambapo watu 85 waliuawa,ambapo pia ofisi ya Rais inatuhumiwa kuwa iliweka mazingira ya kumlinda mtuhumiwa huyo.