Wapiganaji waiteka nyara hoteli Libya

Haki miliki ya picha Other
Image caption Corinthia Hotel

Watu wenye silaha wameshambulia mojawepo ya hoteli maarufu zaidi katika mji mkuu wa Libya-Tripoli.

Inasemekana kuwa walitegua bomu katika eneo la kuegeshea magari kwenye hoteli hiyo ya kifahari ya Corinthia.

Duru za habari zinaashiria kuwa kuna watu ambao aidha wameuawa au kujeruhiwa huku watekaji nyara wakiendelea kuwashikilia watu mateka ndani ya hoteli hiyo.

Walinda usalama wamezingira hoteli hiyo.

Hoteli ya Corinthia ni maarufu sana kwa wafanyibiashara wa kigeni na wanadiplomasia.