Nadal achapwa tennis Australia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rafael Nadal mcheza tenisi nambari tatu kwa ubora duniani kwa wanaume raia wa Hispania

Tomas Berdych ameibuka kidedea kwa kufanikiwa kumchakaza mcheza tenesi nambari tatu kwa kwa ubora duniani upande wa wanaume, Rafael Nadal katika michuano ya tenesi ya Melbourne, nchini Australia.

Berdych alifanikiwa kupata ushindi wa seti 6-2 6-0 7-6 (7-5) mchezo uliotumia saa mbili na dakika kumi na tatu.

Kwa ushindi huo Berdych atakutana na Andy Murray au Nick Kyrgios katika hatua ya nne,mchezaji huyu amekuwa chini ya kocha Dani Vallverdu aliyewahi kuwa kocha wa Murray.

Kwa upande wa wanawake mcheza tenesi nyota Maria Sharapova alimchapa Eugenie Bouchard katika mchezo wa nusu fainali ya wanawake.

Bingwa huyo wa mwaka 2008 alipata ushindi wa 6-3 6-2 katika mchezo uliochezwa kwa saa moja na dakika kumi nane.

Sharapova atacheza mchezo unaofuata dhidi ya Ekaterina Makarova aliyemgalagaza vibaya Simona Halep kwa seti 6-4 6-0.