Wanajeshi wawaua waasi waliojisalimisha

Image caption waasi drc

Wakaazi wa kazkazini magharibi mwa Burundi wameiambia BBC kwamba walishuhudia wanajeshi wa serikali wakiwaua waasi waliojisalimisha.

Wanakijiji wa mkoa wa Cibitoke walisema kuwa takriban waasi 17 walipigwa risasi na kuuawa mapema mwezi huu baada ya kusalimu silaha zao.

Wakaazi baadaaye waliagizwa kuwazika waathiriwa.

Utambuzi wa waasi hao waliovuka mpaka kutoka DRC haujulikani.

Jeshi la Burundi limekana kuchukua sheria mikononi mwao.

Hatahivyo msemaji wa jeshi hilo amesema kuwa waasi hao waliuawa katika vita.