Mikopo yayumbisha uchumi wa Afrika

Image caption Mikopo na kushuka kwa thamani ya safari za Afrika ndio kunahatarisha uchumi wa kanda nzima

Ripoti mpya imeonya kuwa uthabiti wa uchumi wa mataifa yaliyo kusini mwa jangwa la Sahara, unatishiwa na kushuka kwa thamani ya pesa au sarafau ya kanda hio pamoja na ongezeko katika kiwango cha mataifa hayo kukopa pesa.

Taasisi ya kimataifa kuhusu ustawi na maendeleo yenye makao yake mjini London, inasema kuwa hali ya kiuchumi katika kanda hio ni sawa na hali iliyosababisha kiwango kikubwa cha madeni kwenye masoko mapema miaka ya 1990.

Ripoti hiyo inasema kuwa baadhi ya serikali za kanda hio, kama vile Ghana zinafanya hali kuwa mbaya kwa kutumia mikopo kufadhili mishahara ya wafanyakazi wa umma.

Taifa lenye uchumi mkubwa katika kanda hio, Nigeria,imeshuhudia thamani ya sarafu yake ikishuka kwa sababu ya kushuka kwa bei ya mafuta.