England yakufuru usajili wa wachezaji

Haki miliki ya picha AP
Image caption Sepp Blatter rais wa FIFA

Shirikisho la Soka duniani, FIFA, limesema vilabu vya mpira wa miguu vilitumia kiasi cha dola bilioni nne nukta moja katika uhamisho wa wachezaji wa kimataifa mwaka uliopita, ambacho ni kiwango cha juu kabisa kuwahi kufikiwa katika uhamisho wa wachezaji.

England ndiyo iliyotumia kiasi cha juu kabisa duniani, kwa timu zake kulipa dola bilioni moja nukta mbili mwaka 2014.

Vilabu vya Hispania vilishika nafasi ya pili kwa matumizi ya uhamisho wa wachezaji, vikitumia dola milioni mia saba.

Takwimu hizo pia zinabainisha kuwa India ilisajili wachezaji wenye umri mkubwa kuliko wote duniani kwa wastani, na China ikiingia katika kundi la nchi kumi za kwanza katika matumizi ya uhamisho kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo.

Takwimu hizi mpya hazihusishi uhamisho wa wachezaji kati ya timu moja na nyingine ndani ya nchi husika.