Japan yalaani kanda kuhusu mateka

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kenji Goto ni mwandishi wa habari ambaye maisha yake yamo hatarini

Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe, amekitaja kua kitendo kiovu mno cha hatua ya kutolewa kwa kanda nyengine mpya ya video inayomwonyesha raia mmoja wa Japan akiwa ameshikwa mateka na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Islamic State.

Katika kanda hio raia huyo mwandishi Kenji Goto anasikika akisema atauawa katika muda wa saa 24 zijazo.

Sauti nyengine inasikika kwenye kanda hio ikisema Kenji Goto atanusurika tu iwapo Jordan itamwachilia huru mwanamke mmoja mfuasi wa kundi hilo la IS ambae anakabiliwa na hukumu ya kifo nchini humo.

Sauti hiyo hiyo imeongeza kusema kuwa mateka mwengine rubani kutoka Jordan pia anakabiliwa na hatma hiyo hiyo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mamake Goto ameitaka Japana kushauriana na Jordan kuhakikisha mwanawe anaachiliwa huru

Viongozi wa Jordan na Japan wanashirikiana katika juhudi za kutaka kuachiwa huru kwa mateka hao.

Wakati huohuo, mamake mwandishi huyo, amemsihi waziri mkuu Shinzo Abe, kushirikiana na Jordan kuhakikisha mwanawe anawachiliwa.

Kumekuwa na taarifa ya mawasiliano ya siri na kundi hilo kupitia kwa viongozi wao wa kikabila nchini Iraq.

Makataa iliyotolewa na IS inakamilika leo.