Chelsea yatinga fainali Kombe la Capital

Image caption Wachezaji wa Chelsea wakiwa na bango lao wakijinadi kwenda kucheza fainali uwanja wa Wembley baada ya kuwabwaga Liverpool 1-0

Chelsea wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani Stamford Bridge wamefanikiwa kutinga fainali ya kombe la ligi Capital One, baada ya kuwachapa Liverpool bao 1-0.

Dakika tisini za kawaida za mchezo zilimalizika bila ya kufungana ndipo zikaongezwa dakika 30.

Beki Branislav Ivanovic ndiye aliyeipa Chelsea nafasi ya kwenda fainali baada ya kuipatia goli kwa mpira wa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Willian.

Liverpool imeshindwa kuwafunga Chelsea kwa michezo sita mfululizo ya hivi karibuni

Huku Leo Jumatano kutakuwa na mchezo mwingine wa marudiano wa nusu fainali kati ya Sheffield United na Tottenham katika dimba la Bramall Lane

Katika Mechi ya kwanza iliyochezwa wiki iliyopita White Hart Lane, Tottenham iliifunga Sheffield United bao 1-0.

Mshindi wa mchezo huu atachuana na Chelsea katika hatua ya fainaliitakayochezwa Machi mosi katika dimba la Wembley.