Korti yakwaza Google, Yahoo na Microsoft

Haki miliki ya picha AP

Mahakama kuu nchini India imeamrisha kampuni kubwa za internet, Google, Yahoo na Microsoft kubana matangazo ya biashara ya kuwapima wanawake wajawazito ili kubaini jinsia ya mtoto kabla ya kuzaliwa.

Matangazo kama hayo, ni kinyume na sheria nchini India kwa sababu kuna visa vingi vya wanawake kuavya mimba wanapogundua wana mtoto mwenye jinsia wasioitaka.

Hali hii imechochea tatizo la pengo katika jinsia moja kuwa ikilinganishwa na nyingine.

Mahakama ilikuwa inatoa uamuzi katika kesi iliyowasilishwa mbele yake kuhusu kuzagaa kwa matangazo ya biashara ya kubaini jinsia ya mtoto akiwa tumboni kwenye mitandao hio.