Mashindano ya makalio yafanyika Marekani

Haki miliki ya picha bb
Image caption Mwanamke mwenye makalio makubwa

Ni swala la kushangaza kwamba shindano la kumtafuta mwanamke mwenye makalio makubwa mjini New York Marekani litatumiwa kama kigezo cha upasuaji wa mapambo ,huku sheria ya wanawake wanaoruhusiwa kushindana wakitakiwa kuwa ambao hawajafanyiwa upasuaji wowote wa mapambo.

Mwandalizi wa shindano hilo ni daktari Michael Jones ambaye anamiliki kampuni ya mapambo ya upasuaji ya Lexington.

Mbali na kandarasi hiyo ya kumodel mshindi atapata dola 2,000 fedha taslimu.

Gazeti la The New York post limeripoti kwamba wanawake 68 wanashiriki katika shindano hilo.

Wanaoshiriki ni pamoja na model warefu kutoka Washington na mkufunzi wa kibinafsi wa mchezaji densi Brenda Monks ,Chelsea Simone.

Ili kufuzu wanaotaka kushiriki waliulizwa ni kwa nini wanajivunia makalio yao?.

Mwanamke wa miaka 20 Derby Pucket alisema kwamba makalio yake makubwa yanatokana na mazoezi ,ulaji wa kuku,biskuti na chakula kinachompa mafuta mengi.

Mwishoni mwa siku,waliofika fainali walipunguzwa hadi kufika watu 13 ambao watatawazwa mwishoni mwa mwezi huu.