MSF kuondoa wafanyakazi wake Sudan.K

Haki miliki ya picha AFP GETTY
Image caption Hali inayowakabili wanachi wa Sudan Kusini ni ngumu hasa kutokana na vita

Shirika la misaada la madaktari wasio na mipaka MSF linasema kuwa linajiandaa kuwaondoa wafanyakazi wake wa kutoa misaada nchini Sudan kwa sababu maafisa wa serikali wanatatiza juhudi zao katika eneo hilo linalokabiliwa na mizozo.

MSF linasema kuwa serikali inafanya maksudi kutatiza shughuli za wafanyakazi hao na pia kuwazuia kufika katika majimbo ya Darfur na Blue Nile ambako maelfu ya watu wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Jeshi la Sudan linakabiliwa na kibarua kigumu kupambana na waasi katika mpaka wa Kusini mwa nchi.

Wiki jana shirika la MSF lilituhumu jeshi la nchi hio kwa kushambulia hospitali katika milima ya Nuba eneo lengine linalozozaniwa.