Australia kuchunguza Ugaidi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Naibu Kamanda wa Polisi wa Australia Michael Phelan

Uchunguzi mpya umeanzishwa rasmi nchini Australia katika mji wa Sydney kutokana na shambulio la kigaidi lililofanyika katika mkahawa mmoja mwezi uliopita na kuwa kubwa katika historia ya nchi hiyo na lililosababisha operesheni kubwa dhidi ya ugaidi.

Hata hivyo ufuatiliaji huo wa kina ni kufuatia taarifa zilizodai kuwa watu wawili waliouawa mmoja aliyefahamika kwa jina Katrina Dawson alipigwa risasi na polisi.

Ilibainika pia kuwa meneja wa mkahawa huo Tori Johnson alipigwa risasi nyuma ya kichwa na Man Haron Monis mpiganaji wa kundi la Kiislam na mzaliwa wa Iran aliyeuawa na Polisi ndani ya saa 16 za msako wao.

Monis alikuwa mfuasi wa kundi la wapiganaji wa Islamic State, japo kuwa Polisi wa Australia walibaini kuwa alikuwa akitekeleza mashambulio ya kigaidi pekee yake.