Kampuni ya kichina yawafadhili waasi Sudan.K

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mazunguzo ya kumaliza mzozo wa Sudani kusini huenda yakahitimisha mapigano

Shirika la utafiti kuhuhusu silaha ndogondogo, limesema kuwa Kampuni ya mafuta iliyo na mahusiano na China inawafadhili wanamgambo nchini Sudani kusini.

Wanamgambo takriban mia saba wanaelezwa kupelekwa katika maeneo ya machimbo ya mafuta yanayomilikiwa na Kampuni hiyo ambayo Shirika la Petroli la Kenya lina hisa kubwa zaidi.

Hakukuwa na majibu yoyote kuhusu utafiti uliotolewa na Kampuni ya Mafuta.

Katika hatua nyingine, Mkutano wa kanda uliopangwa kufanyika ili kutatua mzozo wa wenyewe kwa wenyewe nchini Sudani Kusini umeahirishwa mpaka jumamosi.

Kulikuwa na Ripoti kuwa Rais wa Sudani kusini ,salva Kiir alikuwa Mgonjwa hali iliyofanya mkutano uanze kwa kuchelewa.

Hata hivyo Maafisa wa Serikali wanasema Afya yake ni njema.