Misri yapiga marufuku tawi la Hamas

Mahakama ya Misri yamepiga marufuku tawi lenye silaha la chama cha Palestina, Hamas, na limewekwa kwenye orodha ya makundi ya kigaidi.

Hamas ina kauli Gaza, na wakuu wa Misri wanadai kuwa tawi hilo linaingiza silaha kimagendo kaskazini mwa Sinai.

Siku chache zilizopita, wapiganaji Waislamu waliuwa watu 30 katika shambulio kubwa dhidi ya polisi na jeshi.

Hamas imelaani uamuzi huo wa mahakama na kusema kuwa ni wa kisiasa