Amnesty International laishtumu Misri

Image caption Waandamanaji nchini Misri

Shirika la haki za binadamu la Amnesty International limeushtumu utawala nchini Misri kwa kufunika mauaji ya watu 27 wiki iliyopita wakati wa mandamano ya kuadhimisha mwaka wa nne tangu kufanyike mapinduzi nchini humo.

Amnesty inasema kuwa ushahidi unaonyesha kuwa vikosi vya usalama vilitumia nguvu kupitia kiasi dhidi ya waandamanaji na wapita njia.

Limeushtumu utawala wa nchi hiyo kwa kushindwa kuwafikisha mbele ya sheria wahusika.

Image caption Vikosi vya usalama vikijaribu kuwadhibiti waandamanaji nchini Misri

Amnesty inasema kuwa jamii ya kimataifa ni lazima ichukue hatua sasa ili kusitisha vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu nchini Misri .

Misri inasema kuwa watu 500 waliokamatwa ni wanachama wa kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brothehood.