AU yahitaji fedha za bajeti

wanajeshi wa AU Somalia Haki miliki ya picha bbc

Katika mkutano wa siku mbili wa viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika, viongozi hao wamependekeza kuanzisha kodi ili kugharimia shirika hilo.

Wamependekeza kodi itozwe juu ya tikiti za ndege, hoteli, na ujumbe wa simu za mkononi.

AU zamani ikifadhiliwa na kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, lakini sasa bajeti yake inagharimiwa na wafadhili wa kimataifa.

Viongozi hao walipokutana mjini Addis Ababa piya walisema kuwa Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC, inafaa kufuta mashtaka dhidi ya rais wa Sudan, Omar al-Bashir, na makamo wa rais wa Kenya, William Ruto.

AU imekuwa ikiilaumu ICC kuwa mara nyingi inawalenga viongozi wa Afrika.