Mwana wa Whitney Houston apoteza fahamu

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bobby Kristina na mamaake Whitney Houston

Mwana wa gwiji wa muziki marehemu Whitney Houston Bobbi Kristina jumamosi alipatikana akiwa kichwa chake kiko ndani ya maji na asiye na fahamu katika beseni la kuogea lililokuwa limejaa maji nyumbani kwake.

Kulingana na shahidi mmoja ambaye ni mtu wa karibu wa familia hiyo, Whitney alikuwa hawezi kupumua baada ya mtu aliyedai kuwa mumewe na rafiki walipompata mda wa saa nne asubuhi katika nyumba yake katika eneo la Roswel Georgia kulingana na maafisa wa polisi wa eneo hilo.

Walitafuta usaidizi wa 911 na kufanya matibabu ya dharura hadi maafisa wa usalama walipowasili na kujaribu kumfanya apumue.

Brown alipelekwa katika hospitali ya North Fulton ambapo anaendelea vyema na matibabu.

Hakuna anayejua kilichosababisha hali hiyo.

Maafisa wa matibabu wanasema kuwa wachunguzi hawajapata ushahidi wowote kubainisha kwamba kilikuwa kisa cha utumizi wa mihadarati ama pombe.

Polisi waliitembelea nyumba hiyo hivi majuzi baada ya mtu kuripoti kwamba kumekuwa na vita na baada ya kupolisi kugonga mlango bila mafanikio waliondoka.