Waasi wa Mali wawateka nyara watu 20

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waasi wa Mali

Waasi Kazkazini mwa Mali wamekabiliana na wapiganaji wanaounga mkono serikali,kwa mda na kuwateka nyara takriban watu 20.

Wapiganaji kutoka kundi linalotaka kujitenga la Tuareg kwa jina MNLA na kundi jengine la waarabu wa Mali MAA walidaiwa kukizunguka kijiji cha Kano takriban kilomita 60 mashariki mwa Timbuktu usiku kucha na kufyatuliana risasi na wapiganaji wanaounga mkono serikali wanaojificha katika eneo hilo.

Miaka miwili baada ya jeshi la Ufaransa kuingia na kuwafukuza wapiganaji ,makundi kadhaa yameendelea kufanya mashambulizi katika eneo hilo.