Boko Haram laushambulia mji wa Maiduguri

Image caption Boko haram lashambulia tena mji wa maiduguri

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria, wameshambulia tena mji wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa nchi.

Walioshuhudia tukio hilo, wanasema walisikia sauti za mizinga, na mapambano makali yanaendelea kusini mwa mji, kati ya washambuliaji na wanajeshi wakisaidiwa na wanamgambo.

Mji huo wa Maiduguri ambao ni mji mkuu wa jimbo la Borno ulishambuliwa juma lliilopita na Boko Haram.

Mji huo ni kati ya miji michache inayodhibitiwa na serikali katika jimbo la Borno na unawapa hifadhi maelfu ya watu waliokimbia maeneo yanayozunguka.