Hati ya amani yasainiwa Sudan Kusini

Haki miliki ya picha d
Image caption Salva Kirr

Rais wa Sudan Kusini , Salva Kiir, na kiongozi wa waasi, Riek Machar, wametiliana saini kuundwa kwa serikali ya kugawana madaraka kuhitimisha vita vya zaidi ya mwaka mmoja.

Makubaliano hayo yamefikiwa katika mji mkuu wa Adiss Ababa, Addis Ababa.wanaume hao wawili wamekubaliana kuhitimisha mapigano na vita vya wenyewe kwa wenyewe mpaka kufikia March tano.

Kwa muda kidogo washauri namna gani ya kuunda mfumo wa serikali ya kugawana madaraka.

Taarifa ambazo BBC haijazithibitisha zinaeleza kwamba Rais Salva Kiir atasalia kuwa Rais wa nchi hiyo na Riek Machar atateuliwa kushika wadhifa wa maakamu wa Rais. Vyama hivyo viwili viliingia kwenye mapigano mara tu baada ya Machar kutimuliwa kwenye

wadhifa wa makamu raisi mnamo mwezi December mwaka 2013.

Mazungumzo kadhaa kama hayo ya kutafuta suluhu yalishindwa kuzaa matunda.