Straus Kahn ahusishwa na ukahaba

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Straus Kahn na mkewe akitoka mahakamani

Aliyekuwa mkuu wa shirika la fedha duniani IMF,Dominique Strauss Kahn ameshtakiwa nchini Ufaransa na mashtaka ya usaidizi wa kuwanunua wanawake ili kushiriki katika sherehe za ngono.

Bwana Straus Kahn ambaye alitabiriwa kushinda uchaguzi wa urais nchini Ufaransa alilazimika kukata harakati zake za kisiasa baada ya kudaiwa kum'baka msichana mmoja msaidizi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Straus Kahn na mwanamke mwandishi aliyedai Kahn alitaka kumbaka.

Ameshtakiwa kwa kuwa katikati ya mtandao wa ukahaba mjini Paris,Brussels na Washington.

Bwana Straus-Kahn amekana kujua kwamba wanawake katika sherehe hiyo walilipwa.

Haki miliki ya picha AFP Getty Images
Image caption Straus Kahn na mwanamke msaidizi ambaye alidai kunyanyaswa kijinsia na Kahn

Mwandishi wa BBC mjini Paris amesema kuwa kesi hiyo ni jaribio la kubadilisha mitazamo ya kimaadili nchini Ufaransa.