Wakaazi watofautiana na jeshi Maiduguri

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption wakaazi waliolazimika kuwa wakimbizi wa ndani kwa ndani katika eneo la Maiduguri nchini Nigeria

Jeshi la Nigeria limesema kuwa limefaulu kusambaratisha shambulio la pili la Boko Haram, juma moja tu baada ya kusambaratisha jaribio jingine la mashambulizi katika eneo la kazkazini mashariki mwa Maiduguri.

Msemaji wa jeshi Meja Jenerali Chris Olukade, amesema kuwa waliwauwa waasi wengi wa Boko Haram katika shambulio hilo la hivi punde, huku wakipata bunduki, risasi na magari yaliyokuwa yakitumika na waasi hao wa Boko Haram.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wanajeshi wa Nigeria

Lakini wapiganaji wa vijijini wameiambia BBC kuwa wanakanusha hilo na kusema wanajeshi waliogopa na kutoroka na hakuna dalili zozote za ndege za kijeshi huko.