Wanyongwa kwa kufanya ushirikina China

Image caption Zhang Lidong

Wanachama wawili wa kundi la ushirikina nchini Uchina wamenyongwa kwa madai ya kumuua mwanamke mmoja katika mkahawa wa McDonald's.

Mwanamke huyo alichapwa na wanachama wa kundi hilo, linalojulikana kama kanisa la Mwenyezi Mungu, baada ya kukataa kuwapa nambari ya simu yake.

Mashambulizi hayo yalitokea katika jimbo la mashariki mwa Shangdong Mei mwaka jana.

Image caption Macdonald

Vyombo vya habari vya Kichina vimesema wanachama hao wa ushirikina waliyouawa ni baba na binti yake.

Kanisa hilo linaamini kuwa yesu alifufuka kama mwanamke wa kichina