Kenneth Kaunda alazwa hospitalini

Haki miliki ya picha
Image caption Aliyekuwa rais wa Zambia Kenneth Kaunda amelazwa hospitalini

Aliyekuwa rais wa Zambia Kenneth Kaunda amelazwa hospitalini mjini Lusaka.

Rais mpya wa taifa hilo Edgar Lungu amemtembelea kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 90 hospitalini.

Kaunda aliliongoza taifa hilo kwa miaka 27 tangu lijipatie uhuru wake mwaka 1964.

Alikuwa mwenyeji wa makundi mengi ya kupigania uhuru na usawa wa watu weusi wakati wake.

Licha ya kuwa kiongozi maarufu,alikashifiwa kwa uongozi wake wa kutumia mabavu.

Lakini Kaunda alikubali kuwacha mamlaka katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1991.