Nusu ya waingereza kuugua saratani

Image caption Mtafiti wa ugonjwa wa saratani

Mmoja kati ya watu wawili nchini Uingereza wataugua ugonjwa wa saratani katika maisha yao wachanganuzi wamesema.

Utafiti wa saratani uliofanywa na shirika moja nchini Uingereza,unasema kuwa makadirio hayo yaliotolewa na mbinu mpya ya kuhesabu pia yanafuta utafiti unaosema kuwa mmoja kati ya watu watatu watapatikana na ugonjwa huo nchini Uingereza.

Utafiti huo unasema kuwa kadri watu wanapoishi maisha marefu,ndivyo watu zaidi wanapozidi kuathiriwa.

Hatahivyo kupunguza uzito na kuwacha uvutaji sigara,kunaweza kuwa na madhara makubwa,shirika hilo limesema.

Habari njema ni kwamba idadi ya watu wanaopona ugonjwa huo wa saratani pia inaongezeka.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Utafiti wa seli za saratani

Kupanda kwa idadi ya watu wanaokadiriwa kuuguwa ugonjwa huo kunatokana na harakati za watafiti kutumia mbinu za kisasa na zenye usahihi mkubwa katika uchambuzi wa hatari ya saratani.

Hatahivyo mbinu mpya na ile ya zamani zinaonyesha uwezekano mkubwa wa watu kuugua saratani nchini Uingereza.

Karibia asilimia 54 ya wanaume huugua saratani ikilinganishwa na asilimia 48 ya wanawake, takwimu hizo zinasema.