Shambulio la 9/11 lilifadhiliwa na nani?

Image caption Zacaria aliyeibuka na madai mapya.

Mfungwa Zacarias Moussaoui, aliyefungwa katika gereza la Colorado ,ambaye picha yake haikuwahi kuoneshwa, ameibuka na madai mapya .

Zacarias Moussaoui ameshatumikia kifungo cha muda wa miaka nane gerezani,Zac ni mwanachama wa kundi la Al-Qaeda ambaye kazi yake kubwa ilikuwa ni ulipuaji majengo na hivi karibuni amedai kuwa baadhi ya wana familia ya kifalme ya Saudi Arabia walisaidia ufadhili wa shambulio la Septemba kumia na moja .

Saudi Arabia tayari imekanusha madai hayo yaliyotolewa na mhalifu huyo na kudai kuwa hayana maana.

Katika mahojiano ya kipekee na mfungwa huyo yaliyofanywa kwenye gereza lililo chini ya ulinzi mkali,Zac amewataja maofisa wa serikali ya Saudi Arabia akiwemo mwana wa mfalme al-Faisal Al Saud,ambaye aliwahi kuwa mkuu wa usalama ambaye anadaiwa kulifadhili kundi hilo la Al-Qaed mwishoni mwa mwaka 1990.

Madai yake hayakuishia hapo, amedai pia kuwa alishawahi kukutana na maofisa wa juu wan chi hiyo huko Afghanistan na kuzungumza na ofisa wa ubalozi wa Marekani nchini humo .

Shambulio la September kumi na moja liligharimu maisha ya watu karibu elfu tatu .

Zac na ofisa huyo wa ubalozi pamoja walitarajiwa kusafiri hadi mjini Washington kutafuta eneo zuri la la kuweka kombora la mashambulizi ambayo kama yangefanikiwa wangeidungua ndege ya air Force One,madai hayo .Zac anadai kuwa aliyafanya chini ya kiapo kikali na hayakuwahi kutambulika.

Moussaoui alikamatwa wiki kadhaa kabla ya utekelezaji wa shambulio la September kumi na moja ,na alikamatwa kwa madai ya kutokidhi vigezo vya uhamiaji na wakati huo wa shambulizi la kigaidi yeye alikuwa jela tayari .Zac alipewa mafunzo ya urubani huko Minnesota na amekuwa akijihusisha na usambazaji pesa kwa mtandao zinazohusiana na kundi hilo la Al qaeda .

Mpango mwingine wa Moussaoui ilikuwa kutekeleza kazi aliyopangiwa ya kurusha ndege aina ya 747 na kuielekeza Ikulu ya Marekani .