Wafanyakazi wauawa Libya

Haki miliki ya picha
Image caption Kisima cha mafuta

Habari kutoka Libya zinasema kuwa idadi kadha ya wafanyakazi katika kisima kimoja cha mafuta wameuawa katika shambulio moja Jumanne usiku.

Afisa mmoja mwandamizi wa kijeshi amesema kuwa watu kumi na watatu wameuawa katika kisima cha Mabrook. Watano ni raia wa kigeni, watatu wakiwa ni Wafilipino na wawili wanatoka Ghana.

Afisa huyo amesema kuwa wote waliouawa walikatwa koromeo, mbali na Mlibya mmoja ambaye alipigwa risasi. Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo, ingawaje taarifa za watu walioshuhudia tukio hilo wanasema watu wenye silaha wakijitangaza kuwa wanachama wa kundi la Islamic State ndio waliohusika na mauaji hayo.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufilipino amesema Wafilipino hao watatu walichukuliwa mateka.