Uganda wapinga madaktari kupelekwa nje

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mwanamke mgonjwa akilala kitandani nchini Uganda

Serikali za Uganda na Trinidad na Tobago zina mkataba wa kushirikiana katika sekta ya afya ambapo Uganda ilikubali kutuma wataalamu wa afya kama vile madaktari na wauguzi wapatao 261.

Haijulikani mshahara wao kwa mwezi utakuwa kiasi gani lakini inatarajiwa kuwa watalipwa donge nono.

Hatua hii ingedhaniwa ingewafurahisha watu wengi,lakini kinyume na hatua hiyo imewakasirisha baadhi ya watu ambao wameamua kuishitaki serikali mahakamani kupinga mpango huo wa madaktari kupelekwa nje, wakidai kuwa Uganda haijitoshelezi kwa wafanyakazi wa sekta ya afya.

Alhamisi,ushirika wa makundi ya kijamii ujulikano kama The White Ribbon Alliance umetoa taarifa kuhusu suala hilo kuhusu afya ya mama wajawazito.

Bi Robina Biteyi mratibu wa kitaifa wa The White Ribbon amesema wanapinga mpango huo kwa sababu, Uganda haijitoshelezi kupeleka wataalam wake nje.