Wapiganaji 27 wauawa Misri

Haki miliki ya picha AP
Image caption misri

Wanamgambo 27 wa kiislamu wameuawa kwenye oparesheni kubwa iyoendeshwa na jeshi la Misri katika eneo la Sinai Kaskazini.

Taarifa zinasema kuwa ndege za helikopta zilitumiwa kuwalenga wapiganaji hao ambao wametangaza kulitii kundi la Islamic State.

Ripoti zinasema kuwa wanajeshi wa Misri baadaye waliwaua kwa kuwapiga risasi wanachama 20 wa kundi hilo.

Kundi hilo linasema kuwa liliwavizia wanajeshi wa Misri mwezi uliopita ambapo zaidi ya wanajeshi 30 waliuawa.