Umoja wa mataifa kuchukua hatua Yemen

Haki miliki ya picha AP
Image caption Raia wa Yemen waandamana kupinga waasi wa Houthi

Baraza la usalama la umoja wa mtaaifa limesema kuwa liko tayari kuchukua hatua zaidi iwapo waasi wa Houthi hawawezi kurudi katika meza ya mazungumzo mara moja kwa minajili ya kuwepo kwa mabadiliko ya kidemokrasi.

Kundi hilo linalodhibiti mji mkuu wa Sanaa limevunja bunge na kuteua baraza la mpito kuchukua mahala pake.

Wanachama wa baraza la usalama wanasema kuwa pande zote ni lazima zirejee kwenye mazungumzo ya umoja wa mataifa ambapo walitaka kuachiliwa mara moja kwa rais wa Yemen, waziri mkuu na baraza la mawaziri kutoka vizuizi vya nyumbani.

Nchi za ghuba zimekuwa zikiomba hatua zaidi kutoka kwa jamii ya kimataifa dhidi ya mzozo ulio nchini Yemen.