Kesi ya Al Jazeera Misri yarejelewa

Oeter Greste, Mohammed Fahmy na Baher Mohamed walipokuwa kifungoni pamoja Haki miliki ya picha Reuters

Wakuu wa mahakama nchini Misri wamesema kuwa marudio ya kesi ya waandishi habari wawili wa Al Jazeera yataanza Alhamisi.

Mohamed Fahmy na Baher Mohamed walikutikana na hatia ya kusaidia chama cha Muslim Brotherhood kilichopigwa marufuku.

Kesi hiyo ilizusha malalamiko kimataifa.

Wafungwa wameshatumika siku 407 gerezani.

Mwenzao, Peter Greste, raia wa Australia ambaye alifungwa nao, alifukuzwa ndani ya nchi juma lilopita.

Jamaa wa Bwana Fahmy wameeleza wasiwasi kuwa bado hakutolewa nchini, ingawa amesamehe uraia wake wa Misri ili apate kufunguliwa.

Yeye ana paspoti ya Canada.

Mke wa Baher Mohamed - raia wa Misri - alisema wanaume hao watatu walifikishwa mahakamani pamoja na ingefaa wangeachiliwa huru pamoja.