Amri ya kutotoka nje yaondolewa Baghdad

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Magari yakiendeshwa usiku mjini Baghdad kufuatia kuondolewa kwa marufuku ya kutotoka nje

Raia kwenye mji mkuu wa Iraq Baghdad wamesherehekea kuondolewa kwa amri ya kutotoka nje ya miaka 12 mjini humo.

Picha kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha watu wakicheza mitaani wakati amri hiyo ilipofikia kikomo usiku wa manane.

Vizuizi kadha navyo vitaondolea kujaribu kurahisisha maisha mjini humo.

Waziri mkuu Haider al-Abadi alitangaza hatua hizo wiki iliyopita kwa lengo la kurejesha mji huo katika hali ya kawaida licha ya kuendelea kushuhudiwa kwa ghasia.

Hii ni baada ya mashambulizi ya siku ya Jumamosi yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 30.