Huwezi kusikiliza tena

Maigizo ya vita vya Liberia London

Liberian Girl ni mchezo wa kuigiza ulioandikwa ukizungumzia vita vya Liberia vya mwaka 1992.

Hapa London mchezo huu umekuwa na mvuto, ukisimulia hadithi ya binti mwenye umri wa miaka 14 anayejifanya kuwa mvulana ili kuepuka asibakwe.

Lakini ameshurutishwa kujiunga na askari wanaoshirikiana na waasi kuipiga vita serikali.

Salim Kikeke ameandaa taarifa hii.