BBC yawatahadharisha juu ya utapeli

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Ukurasa wa mtandao wa BBC Swahili

Idhaa ya Kiswahili ya BBC inataka kuwatahadharisha wasikilizaji na watumiaji wa mtandao wake dhidi ya watu wenye nia mbaya wanaotumia jina la BBC kwa vitendo vya kitapeli.

Kumezuka mtandao bandia unaotumia jina la BBC SWAHILI NEWS kuandika habari za uzushi na kulaghai wananchi kwa habari zisizokuwa na ukweli wala uhusiano na shirika hili la habari.

BBC inapenda kuwakumbusha wasikilizaji na wasomaje wake wote wanaofuatilia habari zake kuwa makini na haina blog ya aina hiyo na kwamba habari zote rasmi zinapatikana kupitia bbcswahili.com au bbc.co.uk/swahili.

Tayari mamlaka husika zimepewa taarifa za vitendo hivyo, BBC hautahusika kwa hasara, athari itakayotokana na mtu kutapeliwa kwa njia iliyoelezwa au nyingineyo ambayo haikutolewa na BBC.

Yeyote atakayehisi mwenendo wa aina hii atoe taarifa kupitia swahili@bbc.co.uk <mailto:swahili@bbc.co.uk> au piga simu 0222 701752.