Marekani itapeleka silaha Ukraine?

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Barack Obama na Angela Markel

Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa Marekani inatafakari kupeleka silaha nchini Ukraine kusaidia kukabiliana na Waasi wanaoiunga mkono Urusi.

Akizungumza katika Ikulu ya White House baada ya mazungumzo na Kansela wa Ujerumani Angela Markel, Obama amesema nia itakuwa kuisaidia Ukraine kuimarisha ulinzi kuliko kulishinda jeshi la Urusi. Lakini amesema ana matumaini kuwa suluhu ya kidiplomasia itapatikana.

“Ubabe wa Urusi umeimarisha umoja wa Marekani na Ujerumani na washirika wetu duniani kote na ningependa kumshukuru Angela kwa uongozi wake imara na ushirika wetu tunapokutana na changamoto hii.Tunaendelea kusisitiza kupatikana kwa suluhu kwa njia ya diplomasia”amesema Obama

Naye Kansela wa Ujerumani Angela Markel haoni kama njia za kijeshi zinaweza kuumaliza mzozo huu.