Ligi Kuu kuweka rekodi matangazo ya Tv

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wayne Rooney wa Manchester United akipambana na Phillippe Coutinho wa Liverpool katika moja ya mechi za premier league

Ligi kuu ya England huenda ikatangaza viwango vipya vya malipo kwa matangazo ya televisheni kufikia pauni bilioni £4.4. Anasema wakala wa kimataifa Jorge Mendes.

Viwango vya haki ya kutangaza katika televisheni katika ligi kuu ya England vimekuwa vikipanda kwa miaka sasa.

Mwaka 2011-13: Malipo yalikuwa pauni za Uingereza bilioni £1.77

Kutoka mwaka 2014-16: yamekuwa pauni za Uingereza bilioni £3

Kuanziaa mwaka 2017-19: malipo ya haki miliki ya kutangaza matangazo hayo yanatarajiwa kuwa pauni za Uingereza £4.4(inakisiwa)

"Namna ambavyo unaweka michezo mchana ili kuendana na soko la Asia. Tunatakiwa kufanya hivyo nchini Hispania."

"Ligi Kuu ya England, inafanya kazi nzuri. Unakuwa na vilabu vilivyo chini katika msimamo wa ligi vikipata pauni milioni £80 katika msimu mmoja. Hiki ni kiasi ambacho vilabu vikubwa nchini Hispania vinapata."

Nilimwambia Mendes kuwa uwezo wa mpira wa miguu kutengeneza thamani kubwa zaidi hakuwezi kuendelea daima. Kwamba fedha za TV ambazo zimemfanya kuwa milionea wa kupindukia lazima zifikie ukomo wake haraka.

Mendes alicheka.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mchezaji wa Aston Villa akibishana na wachezaji wa Tottenham katika moja ya michezo ya ligi kuu ya England

"Skiliza, mpira wa miguu ni mchezo nambari moja duniani," alisisitiza. "unayo michezo mingine kama Formula 1 na NBA, lakini soka ni nambari moja. Watu wanauliza kama tumefikia kikomo. Watakuwa wanauliza kitu hicho hicho katika miaka mitatu kuanzia sasa."

Wataalam wanabashiri ongezeko la asilimia 45%kutoka kiwango cha sasa cha mikataba ya TV ya pauni bilioni £3, kwa gharama zinazofikia kiwango cha jumla cha pauni bilioni £4.4 miaka mitatu kutoka mwaka 2016 na 2019.

Kwa kuwepo wazabuni katika vifurushi saba vya kuonyesha mechi za moja kwa moja, mzunguko wa pili wa mnada umeanza.

Mtangazaji mshirika wa sasa BT imefahamika kuwa wamepua kiasi kuliko mwanzo ilivyokuwa na vifurushi walivyonavyo sasa- ikieleweka kuwa wamepata haki za mechi za Ligi ya mabingwa kutoka msimu ujao.

Hata hivyo, BT na wapinzani wao Sky, ambayo wiki iliyopita walitangaza faida kabla ya kodi ya pauni milioni £527 katika miezi sita kuishia mwezi Desemba, wana hangaika ili kuendelea na kiwango walicho pata, na kuna matarajio makubwa kwamba shirika linalomilikiwa na Marekani la Discovery Network (wamiliki wa Eurosport), na shirika la BeIn Sports lenye makao yake nchini Qatar, huenda nayo yakaingia katika kinyang'anyiro hicho na kuchochea uhasama na kushusha thamani.