Nahodha,Costa Concordia afungwa jela

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Capt.Francesco Schettino ahukumiwa miaka 16 jela

Nahodha wa meli ya Costa Concordia iliyosababisha vifo vya watu watu 32 wakiwemo wafanyakazi wa meli hiyo amehukumiwa kwenda jela.

Kwa mjibu wa hukumu hiyo Nahodha huyo atatumikia kifungo cha miaka 16 jela baada ya kubainika kuwa na makosa ya kuua bila kukusudia.

Francesco Schettino hakuwepo Mahakamani wakati hukumu hiyo ikitolewa. Miaka mitatu iliyopita Meli hiyo ya Costa Concordia iligonga miamba karibu na pwani ya Giglio nchini Italia na kusababisha vifo hivyo.

Hata hivyo Schettino bado anafursa ya kuweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.