Kayla Mueller aliuawa na IS:Marekani

Image caption Kayla Mueller wa Shirika la Misaada raia wa Marekani aliyeuawa na IS

Marekani imethibitisha kuuawa kwa Kayla Mueller mfanyakazi wa mashirika ya misaada aliyekuwa akishikiliwa na wapiganaji wa Islamic State IS.

Familia yake imeelezea kusikitishwa kwake na kifo cha Kayla Mueller na wazazi hao kwa uchungu wameonyesha barua aliyowaandikia enzi za uhai wake mara baada ya kuwekwa kuzuizini na IS. Katika salam zake za rambi rambi Rais Barack Obama amesema msichana huyo amewakilisha vyema taifa lake la Marekani. Kumekuwa na taarifa mbili tofauti kutokana na kifo hicho kwani wakati Marekani inasema bila shaka aliuawa, IS wanasema kuwa Kayla Mueller aliuaawa katika mashambulizi ya anga huko Jordan,Jordan imekanusha madai hayo.