Matumaini kupungua mazunguzo ya Ukraine

Haki miliki ya picha AP
Image caption Viongozi wanaoshiriki majadiliano ya kusitisha mapigano Ukraine

Viongozi wa Ufaransa na Ujeruman ambao wanashiriki katika mazungumzo ya kusaka amani na kusitisha mapigano ya Ukraine wanasema kuwa hakuna uhakika kama watafanikiwa kusitisha mapigano.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujeruman Frank-Walter Steinmeier anasema hakutegemea kuwa ghasia na machafuko yanayoendelea Ukraine yangekwamisha fursa ya kupatikana kwa makubaliano.

Rais Barack Obama amemtaka rais wa Urusi Vladimir Putin kusaini makubaliano hayo ya kusitisha mapigano.

Obama ameongeza kuwa iwapo Urusi itaendelea kufadhili machafuko ya Ukraine uamuzi huo utaigharimu nchi hiyo.