Kiongozi wa Al shabab auawa Somalia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani Admiral John Kirby

Wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon imesema kuwa imethibitisha kuwa shambulio la ndege la wiki iliyopita nchini Somalia dhidi ya magaidi wa Al Shabab lilimuua kiongozi mwandamizi wa wapiganaji hao.

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Admiral John Kirby amemtaja aliyeuawa ni Yusuf Dheeq aambaye alikuwa mkuu wa idara ya upelelezi ndani ya kundi hilo.

Kirby pia amesema hakuna raia yeyote aliyejeruhiwa ama kuuawa katika shambulio hiolo la anga lililofanywa na Marekani dhidi ya Al shabaab kusini mwa mji mkuu wa Somalia Mogadishu.