UN yajiondoa katika vita dhidi ya waasi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption wanajeshi wa DR congo

Umoja wa mataifa umeondoa usaidizi wake katika mpango wa kuwashambulia waasi mashariki mwa DR Congo baada ya serikali kukataa kuwafuta kazi majenerali wawili,msemaji wake amesema.

Vikosi vya umoja wa mataifa havikuweza kujiunga katika mashambulizi kwa kuwa majenerali hao wanatuhumiwa na unyanyasaji wa haki za binaadamu,aliongezea.

Mpango huo wa mashambulizi ulilenga kuwapokonya silaha waasi wa FDLR ambao wanaonekana kama tishio la uthabiti wa eneo hili.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Umoja wa mataifa

Serikali ya DR Congo haijatoa tamko lolote kuhusu hatua hiyo ya umoja wa mataifa.

Awali serikali hiyo ilisema kuwa iliwachagua wanajeshi wake hodari kupigana na FDLR,hivyobasi haitachukua amri kutoka kwa umoja wa mataifa.