NGO DRC zataka MUNUSCO isijiondoe Congo

Image caption Majeshi ya kulinda amani MUNUSCO yaliyopo Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Mashirika mbali mbali ya kiraia nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameomba majeshi ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini humo MUNUSCO kufikiria upya mpango wake kujiondoa kupambana na kundi la waasi la FDLR.

Hapo jana majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa yaliyopo Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo yalitangaza kujiondoa katika operesheni hiyo kwa kushirikiana na majeshi ya serikali ya DRC hadi hapo serekali ya Kongo itakapotengua uteuzi wa majenerali wawili walioteuliwa kuongoza opereshini hiyo.

Kwa mujibu wa MUNUSCO majenerali hao wana tuhumiwa kufanya vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.