Kim Kardashian akiri kujikojolea ovyo

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Kim Kardashian na Kanye West

Mke wa msanii Kanye West nchini Marekani mwana mitindo Kim Kardashian West amekiri kwamba licha ya kuvaa nguo zinazowavutia wengi ulimwenguni yeye hujikojolea katika suruali zake za ndani zinazozuia mikojo.

''Mimi hujikojolea kila mara,ni janga kwa kweli'',.huwa hazina mwanya wa kutosha kuniwezesha kukojoa alisema mwanamke huyo maarufu wakati wa mahojiano na jarida la Love ambapo baadaye alipigwa picha akiwa uchi.

Hatahivyo dadaake Kardashian, Kourtney naye alijotokeza na kusema si Kim pekee anayejikojolea hata yeye pia.

Kim: ''Kourtney alikuwa amezidisha tabia hiyo''Ninakumbuka tulikuwa katika hoteli ya Delano mjini Miami -nadhani hawataturuhusu tena kwenda katika hoteli hiyo.

Je,ushawahi kujikojolea katika suruali yako ya ndani?.kwa maoni yako basi ingia katika mtandao wetu wa facebook katika bbcswahili.