Malema atishia kuvuruga hotuba ya Zuma

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kiongozi wa Chama cha EFF julius Malema

Chama cha siasa nchini Afrika Kusini kimetishia kuvuruga hutuba ya rais kwa taifa kikitaka Rais Jacob Zuma kuwajibika kuhusu ufisadi.

The Economic Freedom Fighters inasema kuwa Zuma lazima aeleze nchi wakati anapanga kulipa fedha za umma zilizotumika katika nyumba yake binafsi.

Wananchi wa Africa Kusini hawatilii maanani hotuba ya nchi ya kila mwaka, kwa hivyo ni juu ya mapambo wala si umuhimu wake

Lakini mwaka huu, Mbunge machachari Julius Malema, ametishia kuvuruga hotuba ya rais Zuma.

Bwana Malema anasema rais lazima aeleze kwa nini amekataa kulipa fedha zilizotumika kwa kutengeneza nyumbani kwake katika kijiji cha Nkandla.

Malumbano yanatarajiwa na kuna uwezekano polisi wataitwa bungeni.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi wanatarajiwa kuwazuia wafuasi wa Malema kuvuruga hotuba ya rais Zuma

Kwa miaka 20 chama tawala ANC kimekuwa kikisherehekea umaarufu wake wa kuwa na wanachama wengi.

Lakini Rais Zuma ameshindwa kutupilia mbali kashfa hio, na Wananchi wa Afrika Kusini wamekerwa na kudorora kwa uchumi na kwa upungufu wa nguvu za umeme kote nchini Hata hivyo baadhi ya wananchi, wanamtaja Bw Malema, na EFF, kuwa mtu anayetumia njia ovyo kupata umaruufu

Lakini wengine wanasema rais anafifisha demokrasia changa ya Afrika Kusini, na lazima kuwajibishwa.