Tiger Woods kupumzika Golf kwa muda

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Tiger Woods mcheza gofu mashuhuri duniani

Mcheza gofu mashuhuri duniani Tiger Woods, amesema hana mpango wa kurudi kwa haraka kucheza mchezo huo baada ya kuandamwa na majeruhi. Wood anatarajia kuwa nje ya uwanja wa mchezo wa gofu kwa mapumziko, kwa muda usiojulikana.

Nyota huyo alijiondoa kwenye raundi ya kwanza ya michuano ya wazi ya bima ya wakulima baada ya kupatwa tena na mkasa wa majeruha. Alikua akicheza michuano ya pili mara baada ya kukosekana uwanjani kwa muda mrefu kwa sababu ya upasuaji wa mgongo.

Kulingana ratiba yake ya kawaida, Woods, mwenye miaka 39, alikua anatarajia kushiriki michuano ya Honda Classic kati ya Februari 26 na Machi 1 mwaka huu.