50 shades of grey ni haramu Kenya

Haki miliki ya picha PA
Image caption Fifty shades of grey

Bodi ya Uainishaji wa filamu nchini Kenya imepiga marufuku usambazaji na uuzaji wa filamu Fifty Shades of kwa madai kuwa inaonyesha mwanamke kama mtumwa wa ngono, ina picha za uchi za mwanamke na kuonyesha mambo ya kimapenzi kwa uwazi.

Bodi hiyo ya kudhibiti filamu imewaonya yeyote atakayepatikana akisambaza filamu hiyo atakabiliwa na shtaka la kueneza sinema zenye kuwaonesha watu watu wakiwa tupu na wengine wakistarehe kwa mifumo tofauti.

Mwenye kiti wa Bodi hiyo Askofu Jackson Kosgey alisema kwamba

"Licha ya kuwa filamu ambayo inaleta taswira ya ngono, kwa picha na sauti, ni moja ya filamu nyingi zinazoendeleza kampeni ya watu kukubali kwamba ngono ni jambo la kawaida tu kwa jamii ilhali huo ni ukiukaji wa haki za kibinadamu kulingana na sheria za Kenya. ‘’

Licha ya onyo hilo mashabiki wa filamu hiyo iliyotokana na riwaya kwa jina kama hilo walisema kuwa wataendelea kuitazama aghalabu kisirisiri majumbani mwao.

Image caption Bango linalotangaza kuzinduliwa kwa filamu ya 50 shades of Grey

Baadhi ya filamu ambazo zimepigwa marufuku nchini Kenya ni: The Wolf of Wall Street (2013)na The Story of our Lives (2013)

Wakati huohuo Kikosi cha zima moto kinasema kuwa kinatazamia ongezeko la kupigiwa simu baada ya kuzinduliwa kwa filamu yenye msisimko kwa watu wazima iitwayo Fifty Shades of Grey.

Kikosi cha zima moto Jijini London (LFB) kinasema kuwa kulikuwa na haja kuwa kuzinduliwa kwa filamu hiyo mnamo Februari 13 kunaweza kuongeza idadi ya watu watakaonaswa na kutiwa pingu la kimapenzi.

Tangu mwezi April mwaka uliopita riwaya ya Fifty Shades of Grey ilipozinduliwa kitengo hicho kimeshughulikia zaidi ya visa kama hivyo vipatavyo 393.

Bodi ya usimamizi wa filamu - LFB inasema kuwa watu wanafaa kutumia busara haswa wanapojaribu mbinu mpya zinazopigiwa debe na filamu hiyo.

''Mara nyingi watu wanapiga simu ya dharura ya 999 baada ya kukwama ama kushindwa kujinusuru kutoka kwa pingu ama minyororo kufuatia vipindi vya ashki na kujamiana.

Filamu hiyo inayotokana na riwaya ya EL James, imeelezewa kuwa yenye visa vingi vya ngono ambavyo kwa baadhi ya wakosoaji, vinadunisha hadhi ya mwanamke katika jamii.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Badhi ya vitu vinavyopendekezwa kukuza mahaba baina ya wapenzi

Inaangazia mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanafunzi aitwaye Anastasia Steele na bwenyenye Christian Grey.

Dave Brown kutoka LFB anasema.

"Madhara ya The Fifty Shades yanaonekana kunaweza kuongeza idadi ya watu watakaonaswa na kutiwa pingu za kimapenzi, sasa tuna matumaini kuwa watu watatumia akili ili kujiepusha na kupagawa kimapenzi.

"nataka kuwakumbusha watu kuwa nambari 999 ni ya dharura na inafaa tu kutumiwa kwa maswala ya dharura"

Katika kisa kimoja zima moto waliitwa na mwanamke mmoja ambaye mumewe ambaye alikuwa amenaswa na mshipi wake kutokana na ashki.

Aidha zima moto mmoja wa kike aliongeza kuwa "ushauri wetu ni kujaribu kujiepusha kabisa kuwa katika hali hiyo."

Riwaya hii imezua mjadala na muamko mpya miongoni mwa wanawake ambao wanasema imeamsha hisia zao mbali na kuimarisha mbinu zao za kujistarehesha.