Afrika Kusini:Vurugu zatanda Bungeni

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wabunge wa upinzani wakitolewa nje ya Bunge na vyombo vya usalama

Bunge la Afrika kusini liligeuka kuwa uwanja wa vita ambapo wabunge wa upinzani ilifikia hatua ya kuvutana mashati na maafisa wa usalama na kufanya wabunge wa upinzani wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) wakiongozwa na Julias Malema kutolewa nje ya ukumbi wa bunge kwa nguvu na baadae wabunge wengine wa upanzani nao wakatoka nje ya ukumbi.

Sakata hilo lilizuka wakati Rais wa nchi hio Jacob Zuma alipokuwa akilihutubia taifa na kuulizwa maswali na wabunge wa chama cha EFF kinachoongozwa na Julius Malema wakitaka kujua ni lini atarejesha pesa zilizojengea jumba lake la kifahari la Nkandla.