Sijawahi jeruhi mchezaji:Costa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mshambuliaji wa Chelsea,Diego Costa amaliza kutumikia adhabu

Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Diego Costa amesema hajawahi kumjeruhi mchezaji mwenzake kwa makusudi mchezoni na kwamba tuhuma hizo dhidi yake ni changamoto anazozipitia na ataendelea kuwa imara. Mchezaji huyo raia wa Brazil mwenye miaka 26 amemaliza kutumikia adhabu ya kutocheza mechi tatu kutokana na kufungiwa kwa kile kilichodaiwa kumuumiza mchezaji wa Liverpool katika mchezo wa nusu fainal mwezi jana. Costa mwenyewe amesema kuwa kuwa hana historia ya mchezo huo mchafu wa kuweza kumuumiza mchezaji mwenzake kwa kudhamiria.

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amelalamikia hatua ya kufungiwa kwa mchezaji wake na kudai kuwa ilikuwa ni tukio la bahati mbaya japo amevituhumu vyombo vya habari kwa kulipa uzito mkubwa Zaidi suala hilo kuliko hali halisi.

Costaaliyejiunga na Chelsea kwa paundi milioni 32 mwezi July mwakajana anasema kuwa amekuwa akichezewa vibaya zaidi na wachezaji wengine matukio yanayowastahili kuchukuliwa adhabu kali kwa makosa kama hayo lakini kwake yeye mambo yanakuwa makubwa zaidi.