Misri kuwaondosha raia wake Libya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption wapiganaji wa makundi tofauti nchini Libya

Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi ametoa ombi la kuwaondosha kwa ndege raia wa Misri wanaoshi nchini Libya,baada ya wapiganaji wa Jihad kuchapisha picha katika mtandao wakisema wamewateka raia 21 wa kanisa la Coptic.

Picha hizo zinaonyesha watu hao wakiwa wamevalia nguo za rangi ya machungwa wakitembezwa katika ufuo wa bahari na watekaji wao walioficha nyuso zao.

Mtandao huo unaoshirikishwa na kundi la Islamic State umewaelezea watu hao kama wana kampeni wa kanisa hilo la Coptic na kusema kuwa kukamatwa kwao ni kulipiza kisasi kile wanachokitaja kuwa utekaji na unyanyasaji wa wanawake waislamu unaotekelezwa na kanisa la Coptic nchini Misri

Waziri wa ,maswala ya kigeni nchini Misri amewataka raia wa Msri kutosafri nchini Libya.